This content is protected.

Punguzeni mechi kitandani-Conte awashauri wachezaji wake

Share this

Mkufunzi wa klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi ya Serie A huko Italia Antonio Conte, amedokeza kwamba huwa anawashauri wachezaji wake kutotumia muda mwingi kufanya mapenzi na wake zao ili kupata muda maalum kushiriki mazoezi na hata kuboresha mchezo wao.

Conte mwenye umri wa miaka 56,aliwahi shinda ligi akiwa na Chelsea mwaka wa 2017 na Juventus huku akijiunga na Inter mwezi Mei.

Miamba hao wa Italia wamefanikiwa kushinda mechi kumi kati ya kumi na mbili walizoshuka dimbani,wakiwa alama moja tu nyuma ya viongozi Juventus.

Image result for CONTE

Matokeo haya yanachangiwa pakubwa na wosia wa Conte kwa wachezaji kupunguza muda wa kushiriki mapenzi na badala yake kutumia muda mwingi uwanjani.

“Wakti msimu unapoendelea,mimi huwashauri wachezaji wangu kupunguza mechi kitandani.” Conte amesema.

Baada ya likizo iliyopisha mechi za kufuzu Euro 2020 ,vijana wake Conte watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya Torino Jumamosi hii.Mashabiki wakisubiri kuona iwapo wosia wa ‘babu’ Conte utakuwa unatumika kisawasawa.

Ukiniuliza nitakuambia kwamba ,Conte ni mkufunzi tena mzazi.

Peter Mokaya

Read Previous

Akothee atoa sababu ya kulazwa hospitalini.

Read Next

Tanzanian Media To Be Fined, Licences Withdrawn For Employing DJs And Comedians

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *