This content is protected.

Nywele halisia ya bindamu:Biashara hii inazalisha mamilioni ya dola katika bara la Afrika,tunaangazia pia siri za ufanisi wa biashara hii

Share this

Iwapo ningekuswali kuhusu mipenyo kumi ya biashara katika bara hili la Afrika,nina uhakika asilimia mia huwezi kuwazia uuzaji wa nyweli halisia ya binadamu kama mojawapo ya nafasi hizo katika ulimwengu wa kuuza na kununua.

Sasa basi,keti kitako usome kwa kumakinika ili uweze kufahamu siri za kutamba katika biashara hii.

Kulingana na makadirio,biashara ya nywele zisizo halisi katika bara la Afrika ina dhamana ya takriban dola milioni sita na biashara hiyo inakua kwa kasi mno.Hivyo basi hili linaweka wazi sababu kuu ya biashara hii kunoga katika solo la bara la Afrika.

Image result for hair styles

Wadadisi wanasema kwamba wanawake wa kiAfrika wanatumia hela maradufu kwa kuremba nywele na vipodozi vingine kuliko wanawake wa Kizungu.

Katika bara ambapo zaidi ya asilimia arobaini ya wananchi wanaishi katika lindi la umasikini,biashara ya urembo hususan uuzaji nywele inazidi kunoga ajabu.

Kila mwaka ,hadhi ya bidhaa za urembo wa nywele katika mataifa ya Nigeria,Afrika Kusini na Cameroon ni dola milioni 1.1.Ifahamike kwamba hii haijumuishi mauzo katika mataifa mengine ya jangwa .

Image result for hair styles

Kulingana na taasisi moja(Euromonitor International),soko la bidhaa za kuremba nywele na hasa zile za majimaji katika bara la Afrika itazidi kukua kwa asilimia tano kati ya mwaka wa 2013-2018.

Sasa basi matini hii haiangazii biashara yote kwa ujumla katika bara hili bali inajikita katika uuzaji wa nywele halisia  ya binadamu ambayo inazalishi mamilioni ya pesa kwa wanabiashara.

Kama utakavyoona katika makala haya,kutokana na hali ya watu wengi kununua nywele hizi,wengi wa wanabiashara wameibuka kuwa wakwasi sana,na la.kushangaza sana ni kwamba wengi wa wanabiashara hawa sio waafrika.

Sasa swali tunalojiuliza sote ni kwamba, mbona wanawake wa kiafrika wameibuka kuzipenda nywele hizi?

Image result for hair styles

Sababu ya kwanza na ya kimsingi kwa biashara hii ya uuzaji nywele halisia kunoga ni kwamba wanawake wengi wanazihitaji.

Na je, mbona wanawake wapo tayari kutumia dola 250 kununua nywele zinazoagizwa kutoka mataifa ya kigeni?

Mwanamke yeyote ambaye ni shabiki wa nywele hizi atakupa majibu take katika misingi hihi:

“Nywele hizi ndio mtindo wa sasa na zinanifanya kupendeza zaidi.”

“Ninapenda kubadilisha mitindo tofauti,na mara nyingi huwa sifurahishwi nikiwa na mtindo mmoja kwa muda mrefu.”

“Nywele yangu ni dhaifu ,hivyo basi inaniwia vigumu kuishughulikia.”

Ili kuwa na usawa kwa kina dada,ni vyema tuwafahamishe kwamba kuna idhibati tosha kwamba nywele iliyo na mguso wa Afro,zina udhaifu na huwa ni vigumu kuzichanua.

Hata hivyo,iwapo ni sawa ama si sawa kwa wanawake wa kiAfrika kutumia nywele hizi zilizoagizwa kutoka mataifa ya kigeni ni mjadala ambao upo nje ya upeo wa makala haya.

Image result for hair styles

Je nywele hizi halisia za binadamu zinatoka wapi?

Katika soko la Afrika,nywele hizi zinapewa majina kutokana na mataifa ambako.ziliagizwa .Kwa mfano,Brazilian,Peruvian na Malyasian .

Ila katika kiwango hiki tutaangazia chimbuko halisi la nywele hizi ambazo zipo kwa wingi katika masoko na vyumba vya urembo barani Afrika.

1. India

Taifa la India ni mojawapo ya wahusika wakuu katika biashara hii wakiwa wanazalisha nywele zenye dhamani ya takriban dola milioni 400 kila mwaka.

India ikiwa na ujumla wa watu bilioni 1.3 huku wanawake wakiwa zaidi ya milioni mia sita ni wazi kwamba sana uwezo wa kuzalisha nywele hizi.

Idadi kubwa ya nywele hizi zinapatikana katika majumba ya kuabudu kwa kile kinachotajwa kama wanawake wengi kukata nywele zao kama njia mojawapo ya kutoa kafara.Na mara nyingi nywele hizi huwa hazijatagusana na kemikali kwa namna yoyote ile.

Mwanamke mmoja anaweza akazalisha gramu 280 ya nywele hizi.Iwapo nywele ni ndefu basi being yake pia huwa juu.Hapo awali nywele hizi zilichomwa ama kutumika katika malazi ila sasa inauziwa kwa wanabiashara mashuhuri na wanao uwezo wa kutoa pesa zinazohitajika.

Baadhi ya nywele hizi zinauzwa barani Afrika na zingine kuuzwa Uropa na taifa la Amerika ambapo pia soko lipo sawa.

Ila ni nywele aina mbili ambazo zinafika Afrika :Remy na Non-Remy.

Image result for remy and rony hair

Nywele ya Remy huwa inakusanywa katika hekalu ,na mara nyingi huwa ina ule uhalisia wake kwa kuwa kila unywele unalenga sehemu sawia.

Aina ya Non-Remy kwa upande mwingine,zinalainishwa kwa kuwa nywele huwa zinalenga sehemu tofauti.Hivyo basi huwa inatibiwa na kemikali (hydrochloric acid) ,ambayo hupunguza hadhi ya nywele hizi kabla hazijasafirishwa hadi Afrika.

Hata hivyo,kutokana na kunoga kwa biashara hii katika taifa la India,kumekua na taarifa za kutisha:

Kwa mfano wanaume wengi wanawashawishi wake zao kuuza nywele zao,watoto wa mitaa wanaahadaiwa na nywele zao kukatwa na kulipwa kwa vidoli,na pia nywele za wafu zinauzwa sokoni.

2. Uchina

Uchina ina idadi kubwa ya wananchi ambayo ni watu bilioni 1.4 ,ambapo asilimia hamsini ni wanawake.Kama India Uchina inachangia kiasi kikubwa cha nywele hii katika soko la dunia kila mwaka.

Kulingana na (World Trade Organization),Uchina iliuza karibia asilia 75 ya manyoya ya ndege,maua yanayotengenezwa na binadamu,na nywele za binadamu ulimwrnguni mnamo mwaka 2012.

Tofauti na India ambapo nywele hizi hupeanwa ka hiari na wanawake,Uchina hii ni biashara mahususi ambapo wanawake maskini huuza nywele zao kwa mawakala katika biashara hii.

Kutokana na ukuzi wa biashara hii,Uchina sasa inauza aina tofauti za bywele hizi ambazo pia hukusanywa kutoka mataifa jirani kama Myanmar,Vietnam,Laos na Bhutan.

Biashara ya nywele katika taifa la Uchina ni kubwa huku wateja wakubwa kutoka Afrika wakiwa:Nigeria,Ghana,Congo,Kenya,Afrika Kusini,Angola na Uganda.

Image result for people selling hair

Hata hivyo wengi wa wanabiashara Uchina wanachanganya nywele hizi na manyoya ya mbuzi ili kuzidisha faida.

3.Afrika Kusini

Inasikitisha kwamba aina nyingi ya nywele zinazouzwa Afrika Kusini huku zikiwa na lebo kama ‘Brazilian’ na ‘Peruvian’ zinatoka Uchina ama India.

Katika kitabu chake ,mtaalamu wa nywele Alix Moore anathibitisha yafuatayo:

“Wananchi wa Brazil hawauzi nywele zao maanake hawaikati ili kupata faida au kutoa kafara katika hekalu hivyo kuwa vigumu kuzalisha nywele katika soko la dunia.”

Kutokana na ununuzi mkubwa wa nywele hizi nchini Brazil,nyingi ya nywele hizi huagizwa kutoka India kila mwaka.

Hii hapa taarifa ya kutisha ya mwanabiashara mashuhuri wa nywele hizi mwenye asili ya kiIndia ambaye anafanyia biashara yake Marekani na ambaye amekua katika biashara hii kwa  takriban  miaka 20:

“Anatumia majina tofauti kwa aina moja ya nywele ili kuwarai watu kuzinunua.”

Nani ambao wanatengeza hela nyingi zaidi katika biashara hii ya nywele barani Afrika?

Wachina na waIndia ndio wanaofaidi pakubwakutokana na biashara hii na wanazoa faida kubwa kutokana na soko la bara la Afrika,huku waAfrika wakiwa chini mwa jedwali miongoni mwa wale wanaofaidi.

Image result for people selling hair

Vifuatavyo ni viwango tofauti ambapo hela huzalishwa:

a) Ukusanyaji wa nywele

Hapa ndipo shughuli nzima inapoanza na mara nyingi wanaohusika kwa asilimia kubwa ni ‘wakusanyaji,’ ambao wanatagusana na nywele hizi kwa Mara ya kwanza kabisa.

Hekalu nyingi hupata hela nyingi kutoka na biashara hii ambapo wanawake wengi hukata nywele zao kwa minajili ya biashara.Hekalu la Tirupathi limejizolea zaidi ya dola milioni 97 tangia mwaka wa 2011.

b) Uzalishaji

Nywele nyingi kutoka Uchina na India hazijachanganywa na bidhaa au kemikali zozote hivyo kuzifanya ziwe na ubora zaidi.Ila kutokana na kuimarika kwa soko,mbinu tofauti zinatumika kutengeneza nywele ambazo zinakaribiana kiasili ili kuzidisha faida.Katika mataifa haya kuna mamia ya kampuni ambazo zinatengeneza nywele hizi.

Image result for china hair

Baada ya kupima na kugawa ,nywele hizi huoshwa na kupangwa kwa vitita vya unywele mia mbili na baadaye kuchanganywa na kemikali kwa siku ishirini  ili kutoa chembechembe zisizohotajika.

Shughuli hizi zote zinaangazia kuongezeka kwa kwa hadhi ya nywele hizi ili mauzo yake yawe ya pesa za juu.

c)Wahusika/Wauzaji

Uzito wa nywele hizi mara nyingi hupimwa kwa toni ambapo toni moja huzalishwa na takriban wanawake elfu tatu.Kila mwaka India wanauza toni 2000 huku Uchina wakiuza zaidi ya hapo.Wanabiashara wengi wa India wametanua mbawa zao katika mataifa ya Afrika.

d) Wanunuzi

Wanunuzi wengi wa Afrika wanashirikishwa katika hatua hii ambapo wengi wao husafiri katika mataifa haya ya kigeni na kuleta nywele hizi ili kuziuza.

Wanunuzi wakubwa wa nywele hizi wapo nchini Nigeria,Afrika Kusini,Ghana na Afrika mashariki huku mizigo ya nywele hizo ikisafirishwa na meli au ndege.

Huku uchumi wa mataifa mbalimbali ukizidi kukua kwa kasi,utandawazi nao ukichukua sehemu kubwa ya binadamu ,ununuzi wa bidhaa hihi kutoka kwa wanawake zaidi ya milioni 400 katika bara la Afrika,biashara hii itazidi kunawiri kila uchao.

Image result for people selling hair

Peter Mokaya

Read Previous

DP Ruto’s Daughter Wants To Be A Teacher

Read Next

Joachim Low:Tumefuzu ila kushinda ni kitendawili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *