This content is protected.

Harmonize kufanya bonge la sajili ndani ya Konde Gang Label

Share this

Tangu aondoke zake WCB,ambayo ni lebo inayotesa kuikweli pale Tanzania,Harmonize anazidi kuthibitisha kwamba mambo yanazidi kunoga kisawasawa katika fani hii ya muziki.

Duru za kuaminika sasa zinadai kwamba Konde Boy atakuwa anafanya usajili wake wa kwanza kabisa ndani ya lebo yake,akitarajiwa kutaja jina la msanii huyo mwanzoni mwa wiki kesho.

Kupitia kwa post yake aliyoachia kwenye Instagram,Harmonize amekiri kwamba ,msanii huyo atakua anasumbua sana kimuziki pale Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Ikumbukwe kwamba msanii huyu aliondoka chini ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz kwa kile alichokitaja kama kutoelewana na baadhi ya miundo au mbinu za kufanya kazi katika lebo hiyo huku akiamua kutanua mbawa na kuhakikisha analea vipaji vya wasanii wengine chipukizi.

Kulishuhudiwa matukio ya kutisha wakati ambapo kulikuwa na tetesi kwamba ,Harmonize alikuwa mbioni kumsajili Alikiba katika lebo ya Konde Gang,jambo ambalo lilionekana kuwa mojawapo ya mbinu kupigana vita kimuziki na Diamond Platinumz.

Msanii huyu ambaye ni sajili mpya  anatambulika kama ‘Young King’ anatarajiwa kuwapa mashabiki burudani la kiukweli,hii ni kulingana na Harmonize mwenyewe.

Usajili huu unajiri siku chache tu baada ya wimbo wake Harmonize kwa jina “UNO” kutolewa katika kitandazi cha youtube baada ya kusemekana kwamba alikuwa kaiba midundo yake producer Magics Enga kutoka Kenya.

Tufanye subira hadi wiki kesho ambapo Harmonize atakuwa anarasmisha na kuweka mambo paruwanja.

Peter Mokaya

Read Previous

Magix Enga Humbles Hamornize Pulling out ‘UNO’ hit from YouTube

Read Next

Mourinho anammezea Gareth Bale

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *