Barcelona yatangaza kikosi chao dhidi ya Leganes

Share this

Miamba wa Uhispania Barcelona wametangaza rasmi kikosi chao kitakachoshuka dimbani dhidi ya Leganes katika kinyanganyiro cha Laliga ugani Butarque Municipal kuanzia saa tisa jioni leo Jumamosi.

Mshambulizi matata duniani na mzaliwa wa Argentina Lionel Messi bila shaka atashirikishwa kikosini,ikikumbukwa kwamba alitia kimiani mabao matatu katika mchuano uliopita dhidi ya Celta Vigo

Arthur Melo ambaye alishiriki katika kikosi cha timu ya taifa Brazil dhidi ya Argentina na Korea Kusini katika michuano ya kufuzu Euro mwaka wa 2020,huenda akakosa kujumuishwa katika kikosi hicho cha Barcelona.

Huenda pia Clement Lenglet akalazimika kula benchi ,licha ya kuisaidia timu yake ya taifa Ufaransa kujihakikishia nafasi  katika kipute cha Euro.

Peter Mokaya

Read Previous

#SHARE MEMES, NOT ANTIBIOTICS, PROCLAIM PHARMACY STUDENTS FROM UON

Read Next

Heads rolling at EastMatt due to public outcry

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This content is protected.