Joachim Low:Tumefuzu ila kushinda ni kitendawili

Share this
                    

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low hana imani iwapo vijana wake watatwaa ubingwa wa kipute cha Euro ambacho kitaandaliwa mwaka kesho(2020),huku akidai kwamba timu kama vile Uingereza,Uhispania,Italia na Ubelgiji zipo na ubora zaidi na zinapigiwa upatu kuibuka kidedea.
Miamba hawa walijihakikishia nafasi yao ndani ya michuano hiyo baada ya kuichabanga Belarus mabao 4-0 hiyo Jumamosi.
Ikumbukwe kwamba kufuzu kwao kunajiri baada ya kusajili matokeo mabovu katika michuano ya kombe la dunia mwaka Jana ambapo walibanduliwa katika awamu ya makundi na timu ya taiga Korea Kusini.
Kumeshuhudiwa pia mchakato wa kujaribisha wachezaji tofauti,jambo ambalo limepelekea wachezaji kama vile Jerome Boateng,Thomas Muller na Mats Hummels wakiwa wanapoteza umuhimu wao katika timu hiyo.Staa wa timu hiyo Mesut Ozil alitangaza kuondokea michuano ya kimataifa kwa kile alichokitaja kama ubaguzi na kukosewa heshima na shirikisho la soka nchini Ujerumani.
Vijana wake Low wameshinda mechi sita kati ya saba katika awamu hii ya kufuzu Euro 2020,huku wakiwa wametia kimiani mabao 24 ila mwalimu huyo anasema vitakua vigumu wao kubeba taji hilo.
Hadi sasa haijafahamika bayana ni wachezaji wapi ambao watashirikishwa,huku Niklas Sule na Leroy Sane ambao wangetumiwa wanahudumia majeraha ya muda mrefu.

Kevin Spahlet

Read Previous

Nywele halisia ya bindamu:Biashara hii inazalisha mamilioni ya dola katika bara la Afrika,tunaangazia pia siri za ufanisi wa biashara hii

Read Next

Togo waibana Harambee Stars nyumbani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This content is protected.